Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.
Katika dunia ya leo ambapo mamilioni ya watu hutegemea utandawazi kupata pesa, kuwa na imani kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua au mtu mwenye nia mbaya na wewe ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa sababu, karibu kila mtu unayekutana naye ni Shetani. Shetani ni mtu yoyote mwenye nia mbaya na wewe. Hivyo, kama uliwahi kuambiwa kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua ni kitu kibaya futa imani hiyo. Utaachaje kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua wakati kila siku unamwomba Mungu akusaidie, na Mungu hutenda kazi zake pale tunapojisahau? La sivyo hutapata pesa unayotamani kupata katika maisha yako, na kamwe hutawaamini watu. Zaka huondoa laana ya mapato. Toa zaka kununua pepo uliyopewa na Mungu.