Loading...
Logo Zenevenes
Login
Logo Zenevenes
  • Home
  • Games

    • Logo Termo/Wordle Termo - Wordle 🇧🇷
    • Logo Termo/Wordle Colmeia - Spelling Bee 🇧🇷
  • Quotes
  1. Quotes
  2. Categorias
  3. mungu
Voltar

Wanasayansi wanasema hakuna Mungu kwa sababu hawawezi kumwona wala kumgusa. Lakini nao hawana akili kwa sababu hawawezi kuiona wala kuigusa.

Enock Maregesi
god intelligence scientists akili mungu wanasayansi

Usiingilie mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu ni dhambi. Dhambi hiyo itakuathiri. Hivyo, jali mambo yako – ya mwingine Mungu anayafanyia kazi – hadi utakapoitwa na Mungu kuingilia kati. Kuingilia kati mambo ya mtu mwingine kunaweza kuathiri mpango wa Mungu katika maisha yake. Hivyo, acha.

Enock Maregesi
life god sin permission god-s-plan mungu dhambi kibali maisha mpango-wa-mungu

Wewe kuingilia mambo ya John ni sawa na kusema, ‘Mungu umeshindwa hebu ngoja na mimi nijaribu; ngoja niingilie kati kukusaidia juu ya maisha ya John Doe.’ Hiyo ni dhambi. Tena ni dhambi kubwa. Unajifananisha na Mungu; kwamba Mungu wa John Doe ameshindwa kwa hiyo mungu wewe ndiye utakayemtatulia matatizo yake. Amri kuu ya kwanza ya Mungu inasema, ‘Usiwe na miungu mingine ila mimi.’ Kuingilia mambo ya John tayari umevunja amri ya kwanza ya Mungu kwa kujifanya Mungu. Mungu ana mpango na maisha ya John, na anatumia matatizo yake kumfikisha kwenye takdiri aliyompangia. Hivyo, wewe si Mungu, acha Mungu afanye kazi yake. Mungu akikuruhusu kuingilia kati, yaani John akiamua kwa hiari yake mwenyewe kukuomba msaada wa mawazo au ushauri, maana yake ni kwamba Mungu amekuchagua wewe kuwa sehemu ya mafanikio ya John Doe.

Enock Maregesi
life god sin help plan mungu dhambi maisha mpango msaada

Mungu ana uwezo wa kukuwekea ulinzi kulia na kushoto yaani anayekulinda naye ana mlinzi wake. Lakini wakati mwingine anaacha ufuate kile ambacho moyo wako unataka kwa sababu hataki kukulazimisha ijapokuwa uwezo huo anao. Mungu hakukuumba kuwa roboti. Alikuumba kuwa huru kuchagua mema au mabaya usije ukamlaumu baadaye kwamba ulimchagua yeye kwa sababu hukuwa na uhuru. Msikilize Roho wa Mungu, kabla na katika kila jambo unalofanya.

Enock Maregesi
god heart defence mungu good-or-evil mema-au-mabaya moyo robot roboti ulinzi

Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.

Enock Maregesi
love friend peace poverty faith pride god enemy fight humans jesus-christ needs battle satan prayers mungu adui imani amani day-of-judgement elects mafuta-ya-dunia-hii majivuno maombi matatizo msalaba-wa-yesu-kristo oil-of-this-world pambana rafiki shetani siku-ya-mwisho tamaa-za-ulimwengu-huu the-cross-of-jesus-christ the-desires-of-this-world umaskini upendo vita wanadamu wateule yesu-kristo

Kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa raha ni rahisi kuliko kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa shida, na utahitaji imani kuendelea kumwamini wakati wa dhiki. Vipindi vigumu katika maisha yetu hutokea kwa kila mmoja wetu. Kuamini ya kwamba Mungu ana makusudi ya lazima kukuondolea vikwazo katika maisha yako ni vigumu sana wakati mwingine, lakini imani ndicho kitu cha muhimu zaidi unachotakiwa kuwa nacho katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Amani ya Mungu, ambayo huzidi hekima na maarifa yote ya kibinadamu, ni kuliamini neno la Mungu kwamba ni la kweli. Bila imani hutaweza kumfurahisha Mungu. Imani ni ufunguo wa nguvu, uwezo na neema ambavyo Mungu ametupangia. Kwa ufupi, Mungu ni mkubwa kuliko wewe na matatizo yako.

Enock Maregesi
life faith god power grace problems key ability comfort-zone difficulty obstacles mungu maisha imani matatizo amani-ya-mungu deliberately dhiki dunia-imekata-tamaa god-almighty makusudi mwenyezi-mungu neema nguvu peace-of-god ufunguo uwezo vikwazo wakati-wa-raha world-has-given-up

Katika dunia ya leo ambapo mamilioni ya watu hutegemea utandawazi kupata pesa, kuwa na imani kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua au mtu mwenye nia mbaya na wewe ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa sababu, karibu kila mtu unayekutana naye ni Shetani. Shetani ni mtu yoyote mwenye nia mbaya na wewe. Hivyo, kama uliwahi kuambiwa kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua ni kitu kibaya futa imani hiyo. Utaachaje kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua wakati kila siku unamwomba Mungu akusaidie, na Mungu hutenda kazi zake pale tunapojisahau? La sivyo hutapata pesa unayotamani kupata katika maisha yako, na kamwe hutawaamini watu. Zaka huondoa laana ya mapato. Toa zaka kununua pepo uliyopewa na Mungu.

Enock Maregesi
life faith god money development world satan paradise tithe mungu maisha malice globalization imani shetani curse-of-income dunia laana-ya-mapato maendeleo mamilioni-ya-watu millions-of-people mtu-usiyemjua nia-mbaya pepo pesa unanimous-person utandawazi zaka

Clique em "Aceitar" para armazenar Cookies que serão usados para melhorar sua experiência, análise de estatísticas de uso e nos ajudar a aperfeiçoar nossos serviços. Saiba mais

Ícone branco Zenevenes
Política de Privacidade | Termos de Uso
Zenevenes.com © 2025