Loading...
Logo Zenevenes
Login
Logo Zenevenes
  • Home
  • Games

    • Logo Termo/Wordle Termo - Wordle 🇧🇷
    • Logo Termo/Wordle Colmeia - Spelling Bee 🇧🇷
  • Quotes
  1. Quotes
  2. Categories
  3. hekima
Back

Mungu hatakubali kuwa na mtu katika ufalme wake ambaye hatakubali kutawaliwa naye. Usikubali kutawaliwa na Ibilisi, kubali kutawaliwa na Mungu. Ni jukumu letu kuanza kuishi sasa kama vile tutakavyoishi mbinguni. Shetani anataka uwe na hekima ya duniani ili akupumbaze. Lakini hofu ya Mungu ndiyo msingi wa hekima ya kweli. Ukitaka asikupumbaze, pokea Roho ya Mungu kwa kubatizwa. Ukiipokea Roho ya Mungu utajua mambo ya Mungu, ambayo dunia haiwezi kujua.

Enock Maregesi
heaven wisdom lucifer kingdom fear-of-god hekima hofu-ya-mungu ibilisi mbinguni ufalme

Mfalme Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kuliko wote ulimwenguni. Anatushauri, “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu (Mithali 25:21-22). Yesu anasema jambo fulani linalofanana sana na hilo katika mafundisho Yake yaliyofuata (Mathayo 5:44-45). Kitendo cha kutukanwa, kupigwa, kushtakiwa au kulazimishwa kubeba mzigo mzito usio wa kwako kinaweza kusababisha mafutu mabaya kabisa katika asili ya binadamu. Yaani, chuki, hasira, ukatili na hata vurugu. Lakini pale wale waliobarikiwa kuwa na hekima wanapojikuta katika majaribu makubwa kama hayo tabia yao haitakiwi kuwa ya shari, inda au ya kulipiza kisasi. Bali inatakiwa kuwa ya kusaidia, kuwa na ridhaa ya kutenda mambo mema, na kuwa mwema kwa wengine siku zote.

Enock Maregesi
wisdom food hatred enemy bitterness anger revenge blessings jesus lord cruelty adversity trials chaos good teachings water hunger doctrine king-solomon hekima adui bwana chakula chuki embers fussiness hasira heavy-load inda kisasi kiu mafundisho mafutu majaribu maji makaa-ya-moto mathayo-5-44-45 matthew-5-44-45 mema mfalme-sulemani mithali-25-21-22 mzigo-mzito njaa proverbs-25-21-22 shari thawabu thirsty ukatili vurugu yesu

Heshima hujengwa kwa hekima, haijengwi kwa misuli.

Enock Maregesi
wisdom respect muscles hekima heshima misuli
Zenevenes white icon
Política de Privacidade | Termos de Uso
Zenevenes.com © 2026