Loading...
Logo Zenevenes
Login
Logo Zenevenes
  • Home
  • Games

    • Logo Termo/Wordle Termo - Wordle 🇧🇷
    • Logo Termo/Wordle Colmeia - Spelling Bee 🇧🇷
  • Quotes
  1. Quotes
  2. Categorias
  3. adui
Voltar

Mfalme Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kuliko wote ulimwenguni. Anatushauri, “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu (Mithali 25:21-22). Yesu anasema jambo fulani linalofanana sana na hilo katika mafundisho Yake yaliyofuata (Mathayo 5:44-45). Kitendo cha kutukanwa, kupigwa, kushtakiwa au kulazimishwa kubeba mzigo mzito usio wa kwako kinaweza kusababisha mafutu mabaya kabisa katika asili ya binadamu. Yaani, chuki, hasira, ukatili na hata vurugu. Lakini pale wale waliobarikiwa kuwa na hekima wanapojikuta katika majaribu makubwa kama hayo tabia yao haitakiwi kuwa ya shari, inda au ya kulipiza kisasi. Bali inatakiwa kuwa ya kusaidia, kuwa na ridhaa ya kutenda mambo mema, na kuwa mwema kwa wengine siku zote.

Enock Maregesi
wisdom food hatred enemy bitterness anger revenge blessings jesus lord cruelty adversity trials chaos good teachings water hunger doctrine king-solomon hekima adui bwana chakula chuki embers fussiness hasira heavy-load inda kisasi kiu mafundisho mafutu majaribu maji makaa-ya-moto mathayo-5-44-45 matthew-5-44-45 mema mfalme-sulemani mithali-25-21-22 mzigo-mzito njaa proverbs-25-21-22 shari thawabu thirsty ukatili vurugu yesu

Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.

Enock Maregesi
love friend peace poverty faith pride god enemy fight humans jesus-christ needs battle satan prayers mungu adui imani amani day-of-judgement elects mafuta-ya-dunia-hii majivuno maombi matatizo msalaba-wa-yesu-kristo oil-of-this-world pambana rafiki shetani siku-ya-mwisho tamaa-za-ulimwengu-huu the-cross-of-jesus-christ the-desires-of-this-world umaskini upendo vita wanadamu wateule yesu-kristo

Clique em "Aceitar" para armazenar Cookies que serão usados para melhorar sua experiência, análise de estatísticas de uso e nos ajudar a aperfeiçoar nossos serviços. Saiba mais

Ícone branco Zenevenes
Política de Privacidade | Termos de Uso
Zenevenes.com © 2025